RBP OIL MDHAMINI MPYA WA AFRICAN LYON, YAMWANGA MIL. 110

RAHMA AL KHAROOS



RAHMA AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA AFRICAN LYON

KAMPUNI ya RBP Oil Industrial Technology Limited imejitokeza kuidhamini timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu Bara iliyoanza leo ambapo imetoa shilingi milioni 110.
Rais wa kampuni hiyo Rahma Al Kharoos alisema ameamua kuidhamini timu hiyo kutokana na kuvutiwa na vipaji ilivyonavyo na pia baada ya timu hiyo kukosa mdhamini baada ya kutemwa na mmiliki wake kampuni ya Mohammed Enterprises.
Lyon imeanza vibayo ligi kwa kufungwa mabao 2-0 na Simba, lakini Rahma amesema itaingia mafichoni kujiandaa na michezo hiyo na anauhakika itafanya vema katika ligi.

Comments

  1. hivi huyu mama mkweli ama msanii, kwa sababu mafedha yake anayotoa ni milioni 100 na kuendelea, isije ikawa shida baadaye, muangalieni huyo

    ReplyDelete
  2. mtu mwenyewe anaonekana 'chopri'lakini ni jambo la kusubiri na kujionea kama ni mkweli ama msanii

    ReplyDelete
  3. mama huyu nampenda sana anaonekana anajali sana michezo hasa soka, big up mama Alkharous endeleza michezo. poa sana

    ReplyDelete

Post a Comment