POULSEN AWATEMA KASEJA, TEGEGE, CHUJI, HUMUD

KOCHA MKUU WA STARS, JAN POULSEN
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza majina ya wachezaji 7 ambao wameachwa katika kikosi cha nyota 26 kwa ajili ya kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012 nchini Benin na Equatorial Guinea ambapo Stars itaanza na Algeria.
Poulsen alisema kwamba, Taifa Stars itaondoka na wachezaji 20 huku akitangaza kuwaa Uhuru Suleiman, Juma Jabu, Jerson Tegete, Juma Kaseja, Abdulhalimu Humoud, Kevin Yondani na Athuman Idd ‘Chuji’ kwa sababu mbalimbali.
Alisema timu yake imejiandaa vyema na michuano hiyo kwa kuwa hadi sasa hakuna majeruhi , na kuongeza kuwa Juma Kaseja ataendelea kukaa benchi kwa wiki moja zaidi hivyo hakukuwa na sababu ya kumpanga.
Watakaowakilisha ni makipa Shaban Hassan (Mtibwa Sugar), Jackson Chove (Azam FC )
Mabeki: Shadrack Nsajigwa (Yanga), Salum Kanoni (Simba), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Stephano Mwasika (Yanga) ,Viungo walioitwa katika kikosi hicho cha Poulsen aliyeanza kazi hiyo Agosti mosi akichukua nafasi ya Mbrazil, Marcio Maximo, ni Henry Joseph (Kongsivinger IL Norway), Jabir Aziz (Azam), na Nurdin Bakari (Yanga).
Wengine ni ,Seleman Kassim (Azam) na Idrisa Rajabu (Sofapaka-Kenya).
Akitangaza majina hayo jana katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ,washambuliaji ni Danny Mrwanda (DT-Long AN-Vetinam), Nizar Khalfan (Vancover White Caps-Canada/USA), Mrisho Ngassa John Bocco (Azam) na Mussa Mgosi (Simba).
Uteuzi huo umekuja baada ya wachezaji hao kufanya mazoezi kwa wiki kadhaa, hivyo amewachuja na kubaki 20 kwa ajili ya kuwakabili Algeria hapo Septemba 3, itakayochezwa mjini Algiers ambapo Stars itaondoka Agosti 31 kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar .

Comments

  1. Aunt Dina hebu tuweke sawa kuhusu mgosi ni kweli yupo AZAM au maandishi yameteteleka tu.

    ReplyDelete

Post a Comment