PATRICK PHIRI ATUA, AWAOMBA RADHI WANASIMBA


KOCHA MKUU WA SIMBA, PATRICK PHIRI

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba Patrick Phiri amewasili nchini na kuwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na kuchelewa kuwasili kwa wakati unaotakiwa.


Akizungumza mara baada ya kuwasili kutoka kwao Zambia, Phiri alisema alikuwa akikabiliwa na matatizo ambapo ilibidi kukabiliana nayo kabla ya kuja nchini.

“Haikuwa kusudio langu kuchelewa kuripoti katika kituo changu cha kazi, hiyo inatiokana na matatizo niliyokuwa nayo ambapo hata Makamu Mwenyekiti (Geofrey Kaburu) alipokuja Lusaka alishuhudia”, Alisema.

Phiri alisema kwamba kutokana na muda wac maandalizi kubaki mchache atajitahidi kuhakikisha anafanya kazi ya ziada ili waweze kuwa imara zaidi na hasa kushinda mechi yao ya kirafiki na Yanga.

Alisema anawafahamu mahasimu wao kuwa wana timu nzuri lakliini ana imani kubwa na wachezaji wake watacheza vizuri na hivyo kuibuka na ushindi siku hiyo.

Phiri leo hii ameungana na wachezaji wa Simba walioko visiwani Zanzibar kujiunga na timu hiyo iliyopiga kambi huko Mbweni nje kidogo ya mji huo ikiandaa na michezo mbalimbali ambapo ilikuwa chini ya kaimu kocha mkuu Syllersaid Mziray ‘mwanangu’ akisaidiwa na Amri Said na Seleman Matola.

Kabla ya kukutana na Yanga Agosti 14, Simba itacheza na mechi ya kimataifa ya kirafiki Agosti nane ikiwa ni maalum kwa kuadhimisha sikui ya Simba ‘Simba Day’, kabla ya kuanza kutetea taji lake la ligi kuu bara itakayoanza Agosti 21 kwa kucheza na Polisi Dodoma.

Comments