"MWANASPOTI MTUOMBE RADHI, BIL 1" VINGINEVYO MAHAKAMANI" -SIMBA

RAGE< MWENYEKITI WA SIMBA
UONGOZI wa klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake Ismail Aden Rage umelitaka gazeti la Mwanaspoti kuomba radhi ndani ya siku 14 pamoja na kulipwa fidia ya shilingi bilioni 1 kinyume na wataliburuza mahakamani.
Hatua hiyo inafuatia gazeti hilo kuandika habari zenye lengo la kuichafua uongozi wa klabu hiyo na hasa mwenyekiti wake kupitia toleo lake la namba 1070 la Agosti 28-30 likiwa na kichwa cha habari “SIKU 11O ZA RAGE NA POROJO ZAKE SIMBA”, RAGE NI NI YULEYULE HAJABADILIKA”.
Akifanua zaidi, Rage alisema katika kurasa za 6 na 8 za gazeti hilo kilichoandikwa humo ni ubabaishwaji wa taaluma ya uandishi wa habari za michezo na uvunjaji wa sheria za nchi kwa sababu ya uvunjaji wa heshima na matusi yaliyoelezwa bila tafsida ya aina yoyote yakielekezwa kwa uongozi wa Simba na mwenyekiti wake.
Awali Rage alisema gazeti hilo limekuwa likitoa taarifa zenye lengo za kuwachonganisha viongozi wa kamati ya utendaji na kundi la marafiki wa Simba ‘Friends of Simba’.
“Mfano kuna taarifa walitoa eti wachezaji wanne wa Simba waliohojiwa kutokana na kudaiwa kuhujumu mechi yetu na Yanga, huo ni uongo kwani kamati haijawahi kukutana kwa ajili ya kujadili kitu kama hicho licha ya mimi kutokuwemo jijini Dar es Salaam, viongozi wenzangu hawakufanya hivyio”.
“Pia linaandika kuwa Friends of Simba wanalipa mishahara ya wachezaji wakati si kweli, sisi tunalipa kwa akaunti zao na hela zao zinatoka kwa wadhamini wetu Kampuni ya bia Tanzania (TBL)”.

Comments

  1. Kwa kweli ninaungana na Bwana Rage japo sii mwana cha wa simba lakini kitaaluma ni mwana sheria. Ni vigumu kuamini kwamba muandishi wa gazeti hilo alitumia AKILI ZAKE timamu wakati akiandika makala hiyo. Na huenda pia alikuwa na ujasiri usio halisi wakati alipokuwa kazini. Ni matumaini yangu kwamba kwa siku zijazo atakuwa akiiwajibisha na kuitumia akili yake pale anapotaka kuandika makala makini itakayosomwa na watu makini.

    ReplyDelete
  2. Kalamu ni silaha nyeti jamani, ukiitimia vyema itakupa mema, na ukiitumia vibaya, mmmh, huleta mabaya. Lengo letu liwe moja, kuitumia kalamu vyema, na watu watuelewe hivyo!

    ReplyDelete
  3. rage acha porojo na vitisho naungana na mwandishi wa gazeti hilo na anakujua fika alichokiandika anakijua,historia yako ipo wazi tangu ulipokuwa katibu mkuu wa tff enzi hizo FAT wizi mlioufanya na ndolanga,moro united waarabu wa watu walikubeba pia ukaharibu,ukarudi TFF upuuzi ule ule simba ahadi kibao hadi leo hewa leo mmkiti wa simba historia itakuja ile ile

    ReplyDelete

Post a Comment