MSAMA AKEMEA WAIMBA INJILI KUTUMBUIZA MAJUKWAA YA SIASA

ALEX MSAMA
MKURUGENZI wa kampuni ya Msama Promotion Alex Msama amekemea mtindo ulioibuka hivi karibuni wa wanamuziki wa Injili kujitokeza kutumbuiza katika majukwaa ya kisaiasa.
Msama amesema wao ni wainjilisti na si wanasiasa hivyo waache kutumika katika majukwaa ya kisaasa sambamba na kushiriki katika kampeni.
Alisema kufanya hivyo ni kumtumikia shetani kwani hawana tofauti na waimbaji wa bongo fleva.

Comments

  1. Dini na siasa ni vigumu kuzitenganisha. Na waimbaji hawa nadhani pia wanajitafutia pesa kwani naamini kwamba wanalipwa na hivi vyama vya siasa ili kutumbuiza katika mikutano hii. Miujiza ya Mungu yaweza tokea na mtu aliyekwenda kusikiliza mkutano wa kisiasa akaishia kumpokea Yesu baada ya kusikia injili ikiungurumishwa.

    Angalia mjadala huu kuona kwamba baadhi ya waimbaji hawa wa injili wapo tu ili kujitafutia pesa na si vinginevyo...

    http://nyimbozadini.blogspot.com/2010/07/ujumbe-na-angalizo-kutoka-kwa-dada.html

    ReplyDelete

Post a Comment