MKWASA ATANGAZA 24 WA TWIGA STARZ WATAKAOKWENDA AFIKA KUSINI

KOCHA MKUU WA TWIGA STARS CHARLES MKWASSA AKITANGAZA WACHEZAJI WA TIMU HIYO WATAKAOKWENDA AFRIKA KUSINI KUSHIRIKI MASHINDANO YA WANAWAKE YA AFRICA MWEZI OKTOBA.

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake, Charles Boniface Mkwassa jana alitangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoanza kujifua leo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Afrika kwa wanawake yanayotarajia kuanza Oktoba nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkwassa alisema amewaandalia program maalum ya mazoezi ya Twiga ambayo ni ya kasi, nguvu na mazoezi ya Gym ambako watakuwa wakifanya mazoezi mara tatu kwa siku.
Mkwasa alisema mazoezi hayo ya Gym yatafanyika asubuhi hadi saa tano kabla ya jioni kuingia uwanjani.
Aidha Mkwasa alitaja kikosi cha wachezaji hao ni pamoja na Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaid Tamba, Fatuma Bushiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamis Omar, Pulkeria Charaji, Esther Chabruma, Hellen Peter, Fridian Daud na Zena Khamis.
Wengine ni Etto Mlenzi, Mary Masatu, Fatuma Khatib, Maimuna Said, Fadhila Kigalawa, Neema Kuga, Mwasiti Ramadhani, Zuhura Kabulule, Mariam Azizi, Fatuma Mustafa, Evelin Kubo na Elizabeth Komba.
Mkwasa alitoa wito kwa wachezaji wa Twiga kuonyesha uzalendo katika mashindano hayo kwa sababu posho walizokuwa wakidai kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), zimeshalipwa.
Mkwasa alisema wakati wakijiandaa na mashindano ya Afrika Twiga itajipima kwa michezo minne kati ya timu ya Taifa ya Afrika Kusini Banyana banyana itakayochezwa Septemba 29 na Oktoba 2 wakati timu ya Taifa ya Zimbabwe watacheza Oktoba 6 na 10.

Comments

  1. Dada Dina niambie kwani najua wewe ni mwana michezo ktk hawa wa dada wote 24 hamna hata mtoto wa wachezaji kandanda wa zamani?

    ReplyDelete

Post a Comment