MKURUGENZI TIC AWAFUNDA WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA

WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010, wametakiwa kutumia nafasi zao kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuweza kuingiza pato la nchi.


Rai hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na mlezi wa Miss Tanzania, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel ole Naiko, alipokuwa akizungumza na warembo hao katika Hoteli ya Giraffe.

Alisema, licha ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya kuwafanya wawekezaji waje kuwekeza, inakuwa ngumu kutokana na kutopata taarifa za kutosha kuhusiana navyo, hivyo ni fursa za warembo hao kutumia nafasi zao kuvitangaza.

Warembo 30 waliopiga kambi ya kujiandaa na shindano hilo, wanatarajiwa kuondoka leo kwenda miji ya Arusha, Moshi na Tanga kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii na kujifunza kwa siku tisa.

Warembo hao ni pamoja na Irene Hezron, Bahati Chando, Christina Justine, Fatma Ibrahim, Magreth Godson, Alice Lushiku, Furaha David, Bunduri Ibrahim, Salma Mwakalukwa, Angelina Ndege, Wande Masegense, Mary Adam na Shadya Mohammed.

Wengine ni Consolata Lucos, Britney Urassa, Marry Kagali, Rachel Sindbard, Flora Martin, Willemi Etami, Anna Daudi, Esther Dennis, Jhally Moray, Amesuu Maliki, Pendo Sam, Prisca Mkonyi, Genevove Emmanuel, Beatrice Premsingh, Glory Mwanga, Flora Florence na Pili Issa.

Comments