MECHI YA NGAO YA HISANI BAINA YA SIMBA NA YANGA SASA AGOSTI 18




SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), limesogeza mbele mchezo wa Ngao ya Hisani baina ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba na mshindi wa pili Yanga kutoka Agosti 14 hadi 18.


Akizungumza na waandishi wa Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kutokana na wachezaji wa Simba na Yanga kuwa katika timu ya Taifa.

Kaijage alisema mchezo huo ni kwa ajili ya kuikaribisha Ligi Kuu Tanzania bara inayotarajia kuanza Agosti 21.

Comments

  1. hili ndio game la ukweli, tunalisubiri kwa hamu kwa sababu Yeboyebo Yanga wanajidai kwa ushindi wao mwembamba na Wamalawi. tunawasubiri kwa hamu

    ReplyDelete
  2. Yanga lazima walale katika mechi hiyo kwa sababu Phiri amerejea, watarajie kichapo na si kingine

    ReplyDelete
  3. Hello Dina hizi habari sijaziona ktk gazeti hata moja yaliomo ktk net sasa kama ni kweli basi mtandao wako na wa cnn hamna tofauti

    ReplyDelete
  4. Tunapenda sana kucheza mdomoni, hapo wameshashinda timu fulani hata kabla ya mchezo, ukichezwa je?

    ReplyDelete
  5. James hujaziona habari zipi, mechi ya ngao ya hisani kweli imesogezwa mbele, mimi ni mwandishi kitaalum sibahatishi wala kukurupuka

    ReplyDelete

Post a Comment