LIGI BARA YAANZA KWA SIMBA, YANGA KUSHINDA

WACXHEZAJI WA SIMBA WAKISHANGILIA MOJA YA BAO
LIGU kuu ya Vodacom imeanza rasmi leo ambapo mabingwa  watetezi wa ligi hiyo Simba imanza kwa kutetea  taji lake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, huku mabo yote ya Simba yakifungwa na Amir Maftah.


Ushindi huo umeiwezesha Simba iliyo chini ya Kocha wake Patrick Phiri, kuanza vema kampeni ya kutetea ubingwa wake iliyoutwaa kwa rekodi ya kushinda mechi 20 na sare mbili.

MECHI NYINGINE:
YANGA Vs POLISI DODOMA 1-0
AFC VS AZAM FC 0-2
KAGERA SUGAR VS JKT RUVU 1-0
TOTO AFRICAN VS RUVU SHOOTING 2-0
MAJIMAJI VS MTIBWA SUGAR 0-1
Ligi hiyo itasimama hadi Septemba 11 kupisha kambi ya tinmu ya Taifa inayojianda na mechi yake dhidi ya Algeria ikiwa ni kampeni ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika

Comments

  1. hawa ndio Simba bwana!!! wameanza ligi kimtindo, kama kawaida ushindi tena msimu huu kama kawaida

    ReplyDelete

Post a Comment