KILIMANJARO LAGER MDHAMINI MPYA BONGO STAR SEARCH

KUTOKA KUSHOTO NI MENEJA WA BIA YA KILIMANJARO GEORGE KAVISHE, MKURUGENZI WA BENCHMARK PRODUCTION RITA PAULSEN


KAMPUNI ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro imeingia mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini shindano la kukuza vipaji vya muziki la Bongo Star Seach (BSS).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema wameamua kudhamini shindano hilo ili kuendeleza mikakati yao kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana.
Alisema udhamini wao kwa mwaka huu utagharimu zaidi ya shilingi milioni 100 ambazo zitatumika katika awamu tofauti ya shindano hilo.
“Kama mjuavyo TBL tunakauli mbiu yetu ya kuwafikisha Watanzania katika kilele cha mafanikio, sasa kupitia BSS tunataka kufikisha vipaji vya washiriki katioka kilele cha mafanikio”, Alisema.
Naye mkurugenzi wa Benchmark Production inayoratibu shindano hilo Rita Paulsen alishukuru kwa udhamini huo na kuahidi kuliboresha zaidi shindano hilo sambamba na kuongeza zawadi kwa washindi.
Taji la shindano hilo linashikiliwa na Pascal Cassian wa Mwanza ambaye kwa sasa amejikita zaidi katika muziki wa injili.

Comments

  1. poa sana, mambo hayo ndio yanatakiwa kwa sababu Bongo Star search ndio chimbuko la muziki ambalo limejipanga vilivyo kwa ajili ya muziki, wasaidieni wajameni

    ReplyDelete

Post a Comment