KIFAHAMU KITUO CHA CHIMBUKO LA UTAMADUNI KILICHOPO MAJOHE






DAVID KITOLERO, MKURUGENZI WA KITUO HICHO


KITUO ambacho ni chimbuko la Utamaduni na utafiti kilichopo Majohe, Gongolamboto jijini Dar es Salaam ni mojawapo ya vituo vichache vya Utamaduni vilivyopo nchini.
Kituo hicho kinaongozwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wizara ya Utamaduni masuala ya Mila, David Kitolero ambaye amejipanga kuboresha na kuendeleza sanaa hapa nchini.
Kituo hicho kitakuwa ni kwa ajili ya  utafiti na maendeleo ya sanaa sambamba na kundi mojawapo la sanaa ambalo litakuwa kituoni hapo kwa ajili ya kufikisha ujumbe.
Amefanikiwa kujenga majengo machache ambayo yamekamilika kwa kiasi fulani ambako ametoa wito kwa wadau wa fani hiyo kumsaidia ili kufikia lengo ambalo litaifikisha mbali tasnia hiyo.
Atakuwa akifundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni utoka nje ya Tanzania, kuchambua makabila mbalimbali ya Tanzania.
Kitolero katika kinyang'anyiro cha kuwania ubunge alijitosa jimbo la Ulanga lililokuwa likishikiliwa na Celina Kombani ambako aliangukia pua na kuangushwa na Kombani. 

Comments

  1. Huyu mzee ni noma katika masuala ya sanaa kwa sababu alikuwa Mkurugenzi wa Utamaduni Mila wa Wizara ya habari Utamaduni na Michezo

    ReplyDelete

Post a Comment