KATUNI DAY NDANI YA CLOUDS FM KESHO, POWER BREAKFAST USO KWA USO NA WAKUDATA

                       

                         MTAYARISHAJI WA KIPINDI CHA POWER BREAKFAST   CHA    REDIO CLOUDS JIMMY FRANCIS KATI, MUSSA NGARANGO KULIA NA SAID MICHAEL KUSHOTO

JIMMY KUSHOTO NA SAID MICHAEL KULIA


HAPA AKIMUHOJI MUSSA NGARANGO

MTAYARISHAJI wa kipindi cha Power Breakfast cha redio Clouds, Jimmy Francis leo ametembelea katika chumba cha hari cha kampuni ya Free Media limited inayochapisha magazeti ya TANZANIA DAIMA na lile la michezo SAYARI na kufanya  mahojiano na wachora katuni wa kampuni hiyo Said Michael  mwenye katuni maarufu ya 'WAKUDATA' na Mussa Ngarango  anayechora katuni ya 'KISUNGURA'.
Katika mahojiano hayo mtayarishaji alitaka kujua masuala mbalimbali ikiwemo  nafasi ya katuni katika jamii na nini wanachokifanya kabla ya kuchora, matatizo yanayowapata na tofauti ya katuni na habari na mambo mengine mengi.
Mahojiano hayo yatasikika kesho katika kipindi cha POWER BRAKFAST ambacho hurushwa kila siku za jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tatu asubuhi chini ya watangazaji wake Babra Hassan, Gerald Hando na Paul James.

Comments