BALOZI WA REDD'S KUSAKWA MWAKA HUU




KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd's Original wanatarajiwa tuzo ya Balozi wa Redd's kupitia mashindano ya Miss Tanzania 2010 yatakayofanyika Septemba 11 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Meneja chapa wa Redd's Original Kabula Mshimo alisema utaratibu na mchakato wa kumchagua Balozi wa mitindo wa Redd's 2010 utakuwa ni ule ule wa jopo la majaji watano litafanya uteuzi huo.
Nsimo alisema mmoja wa majaji hao atatoka Kamati ya Miss Tanzania (LINO), wengine watatoka TBL ambao watatangazwa baadaye.
Nshimo alisema Zawadi atakayonunikiwa Balozi wa Redd's wa mitindo ni sh. 250, 000 kila mwezi kwa kipindi kisichozidi miezi 12.
Alisema vile vile Balozi huyo atahusishwa nakazi mbalimbali za Redd's na TBL kwa ujumla hivyo kumuwezesha kupata kipato zaidi.
Mshindo huo atatangazwa siku ya fainali ya Vodacom Tanzania 2010.
tuzo hilo, ilianza kwa mara ya kwanza Redd's kudhamini Miss Tanzania mwaka 2oo5.
Mshimo alisema alisema aliyeanza kushiriki taji hilo, alikuwa Natalia Yatera ambaye alikuwa msindi wa pili wa Ocean Sandals Miss Tanzania 2005 na mshindi wa tuzo ya Miss Photogenic katika mashindano hayo.
Alisema aliyefuatia kwa kunyakua taji hilo ni Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mshindi wa pili wa Vodacom Miss Tanzania 2006 akifuatia na Victoria Martin aliyekuwa mshindi wa nne wa Vodacom Miss Tanzania 2007 na 2008 alikuwa Angela Lubala ambaye alikuwa mshindi wa pili wa mashindano hayo.

Comments

  1. Siku hizi akina dada mshindwe wenyewe kupata mitaji ya maisha

    ReplyDelete

Post a Comment