DALALI AITAKA SIMBA IWAPE RAHA



HASSAN DALALI 'FIELD MARSHAL'


KIKOSI CHA SIMBA

ALIYEKUWA mwenyekiti wa klabu ya Simba Hassan Dalali 'Field Marshal'amesema ana imani na wachezaji wa klabu hiyo kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwafunga mahasimu wao wa jadi katika mechi yao ya kuwania ngao ya hisani keshokutwa.

Dalali alizungumza nami kwa njia ya simu na kusema kwamba  hata viongozi waliopo katika klabu hiyo wana uwezo mkubwa wa kuhakikisha wanatoka kifua mbele katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

"Nawaomba vijana wetu watupe raha kwa kushinda kwani nina imani kuwa uwezo huo wanao, nawatakia kila la heri katika mechi hiyo na tupo pamoja", Alisema

Comments