ALBAM YA SAJNA SOKONI KESHO, INAITWA 'IVETA' MSIKOSE


SAJNA

COVER ITAKUWA KAMA HIVI

Hello, asante sana kwa mchango wako wa aina yoyote uliotupatia katika kuifanikisha album ya Sajna mpaka kukamilika na sasa ikiwa tayari kuingia sokoni Alhamisi hii tarehe 19 Agosti 2010, ASANTE SANA..

ALBUM TITLE: IVETA
ARTIST: SAJNA
RELEASE DATE: 19TH AUGUST 2010
EXECUTIVE PRODUCER: KID BWOY
DISTRIBUTOR: GMC & UMOJA AUDIO VISUAL
ALBUM DETAILS:
Album ya IVETA ya msanii SAJNA ina jumla ya nyimbo 10, ambayo ilianza kutengenezwa Mwezi January 2010 na kukamilika mwezi July 2010. Wasanii waliopata nafasi ya kushirikishwa katika album hii ni Belle 9, Linah wa THT, Josefly kutoka Musoma Mara pamoja na Pipi. Lengo la kutoshirikisha wasanii wengi sana ni kutaka kuonesha uwezo wake na kuthibitisha kwamba msanii mchanga si lazima atoke kwa kupitia mgongo wa wasanii wakubwa.

Studio na producers waliohusika kutengeneza nyimbo katika album hii ni pamoja na TETEMESHA RECORDZ chini ya KID BWOY, AB RECORDS chini ya AMBA, A2P chini ya SAM TIMBER, IMMORTAL MUSIC chini ya TRIS na M LAB chini ya DUKE.
Single ya pili kutoka bado haijaamuliwa ila ni kati ya SITAKI KUUMIZWA na MBALAMWEZI, moja kati ya hizo itakayopendekezwa na wadau wengi ndio itakayofuata baada ya IVETA.

Song list as appeared on Cd cover
1. IVETA
2. Sitaki Kuumizwa ft. Linah
3. Binadamu
4. Mbalamwezi
5. Udehule
6. Mganga ft. Josefly
7. Nadhifa
8. Roho Mbaya ft. Belle 9 & Pipi
9. Subira
10.Ishara ya Msalaba
ALBUM ITATOKA KATIKA CD NA AUDIO CASSETTE
Regardz
Executive Producer
Kid bwoy
Tetemesha Recordz

Comments

  1. Hongera sana, kama wezi wa kazi zenu usingekuwepo mngekuwa mbali sana, lakini unaweza kukuta album yako ipo mitaani hata kabla hujaizindua

    ReplyDelete

Post a Comment