VODACOM FOUNDATION YADHAMINI ONYESHO LA FASHION 4 HEALTH


MBUNIFU WA MAVAZI MUSTAFA HASSANALI WA PILI KULIA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI KUHUSIANA NA ONYESHO HILO


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation imedhamini onyesho la mavazi ya hisani ‘Fashion 4 health black and Gold Gala’ linalotarajiwa kufanyika julai 30 katika hoteli ya Serena Inn iliyopo Visiwani Zanzibar.

Mustafa Hassanal mbunifu wa mavazi kwamba onyesho hilo ambalo limeandaliwa na Explore Zanzibar litakalokuwa mahususi kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia kuboresha hospitali ya wenye matatizo ya akili iliyopo Visiwani Zanzibar.
Alisema katika onyesho hilo pia anatarajia kuzindua ubunifu wake mpya ujulikanao kama ‘Karafuu’vazi yake pia litasahusisha ambapo wabunifu kutoka Dar es Salaa na Zanzibar watashiriki.

“Ikiwa hii ni mara yangu ya tatu mfululizo kushiriki katika maonyesho ya kuchangia ukarabati wa hospitali hiyo, kwani naamini na sisi tunalo jukumu la kusaidia watu wasiojiweza”, Alisema.

Mbali na Vodacom, onyesho hilo litakaloopambwa na bendi ya Tanzanite, pia limedhaminiwa na PSI, Africa Life Assurance, Explore Zanzibar, 361 degrees events, Vayle Springs na Mustafa Hassanali Couture.

Comments