TBL YAIPIGA JEKI TASWA FC



KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imeipatia shilingi  4.8 timu ya soka Waandishi wa Habari za Michezo ‘TASWA FC’ inayotarajiwa kushiriki bonanza la waandishi wa habari litakalofanyika jumapili mjini  Arusha.


Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa TBL, Edith Mushi, alisema wametoa fedha hizo baada ya kutambua mchango wa waandishi wa habari za michezo.

Mushi alitoa wito kwa wachezaji wa timu hiyo, kurejea jijini Dar es Salaam na taji la ushindi kama ilivyokuwa mwaka jana.

Aidha, aliwataka waandishi hao kutangaza vema bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo katika bonanza hilo.

Naye Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omar, alitoa shukrani kwa msaada huo na kuahidi kurejea na ushindi katika bonanza hilo.

Omar alisema ti

Comments