STEVE NYERERE AWA KAMANDA WA VIJANA BWAWANI



Kamanda mpya wa Vijana CCM Tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele Nyerere, akiongea na wana CCM. mara baada ya kutawazwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa kata hiyo leo kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za tawi hilo na kuhudhuriwa na wanachama wa chama hicho, pamoja na marafiki wa msanii huo anayeigiza sauti za viongozi. "Steve Nyerere" amewashukuru marafiki zake, wazee wake mtaani, mama zake pamoja na mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Ritah. ambaye amemtania kwamba anaongea sana hivyo anaweza kuanzisha chama cha kuwasuta watu na kikawa kizuri sana, lakini pia hakusita kumshukuru mke wake na kumtania kwamba leo walipoamka asubuhi alimsalimia kwa kumtania na kusema "Mambo Kamanda naye Steve Nyerere akajibu Poa mke wangu" Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Mkoani Mara na mgeni rasmi .


Bw. Domi Athman Juma akimvisha joho Kamanda mpya wa vijana wa tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele maarufu kama Steven Nyerere leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika tawini hapo na kuhudhuriwa na wanaccm mbalimbali wa kutoka tawi hilo.



Mtoto wa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi Abbs Mwinyi akiongea katika mkutano huo mara baada ya kuchangia fedha ambazo hakutaka kutangaza kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kamanda wa vijana wa Tawi hilo amabaye amesimikwa leo kulia ni. mgeni rasmi Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Moa wa Mara Domi Athman Juma

Comments