SIMBA YAWAPIGIA CHAPUO MZIRAY 'MWANANGU', TIMBE

MWENYEKITI WA SIMBA, ISMAIL ADEN RAGE KULIA na OFISA TAWALA WA SIMBA EVODIOUS MTAWALA

KATIKA kuimarisha benchi lake la ufundi, uongozi wa Simba upo katika mazungumzo na makocha wazoefu Sam Timbe wa Uganda na Mzalendo Syllersaid Mziray 'Mwanagu'.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Adenm Rage amesema kwamba mmoja kati ya hao watakayeafikiana naye basi atafanya kazi pamoja na kocha mkuu wa sasa Patrck Phiri wa Zambia ambaye anatarajia kuwasili Julai 12 akitokea kwao kwa mapumziko.


RAGE, MTAWALA
Alisema wachezaji wa Sinmba wameanza mazoezi ya kujenga miili yao 'GYM' ambapo baada ya kuwasili kwa Kocha Phiri wataingia kambini rasmi katika kambi itakayopigwa nje ya jiji la Dar es Salaam.

Comments

  1. dina hongera kwa kuwa na blog nakusoma dada unajitahidi kuweka picha, mwaaaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete

Post a Comment