SIMBA YAJIPANGA KWA SAFARI YA UFARANSA

RAGE, MWENYEKITI WA SIMBA

WAKATI wakala aliyezialika Ufaransa timu za Simba, Yanga na Azam akitarajiwa kuwasili nchini Jumatatu ili kuweka mambo sawa, klabu ya Simba huenda ikafaidiaka zaidi baada ya kuwa karibu zaidi na wakala huyo.


Habari zilizopatikana toka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kuwa Simba ndio itakuwa mwenyeji wao hapa nchini baada ya kumtumia tiketi ya kuja nchini kama alivyowataka.

Mmoja ya viogozi wa Simba alisema jana kwamba wakala huyo ameipa kipaumbelea zaidi timu yao kutokana na viongozi wake kuonyesha nia madhubuti nya kuukubali mwaliko huo.

“Sisi baada ya kupewa taarifa tulithibitisha kuwa tutahudhuria na tumekuwa na mawasiliano kiasi cha wakala huyo kuomba tumtumie tiketi ya kuja huku kwa ajili ya makubaliano ya mwisho, tulifanya hivyo na anakuja Jumatatu”, Alisema.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa wachezaji 20 na viongozi watano wanatarajiwa kuwemo kwenye ziara hiyo itakayokuwa kati ya mwezi huu na Agosti ambapo timu zitapata fursa ya kucheza mechi za kirafiki na timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo maarufu kama ‘League 1’ zikiwemo Rens, Nice, Life, Auxerre, Soux na nyinginezo.

Katika hatua nyingine Yanga imerudisha nyuma mazoezi rasmi ya wachezaji wa timu hiyo kutoka Julai 15 hadi kesho ili kujiandaa na safari hiyo, imefahamika.

Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu alisema jana kwamba wamepata taarifa kuwa wakala huyo atawasili ijumaa hivyo hawana budi kujiandaa iliu kujiweka tayari kwa safari hiyo ambayo anaaminini itakuwa na manufaa makubwa kwa timu hizo.

Comments