SIMBA, AZAM NA YANGA ZAALIKWA UFARANSA


KIKOSI CHA SIMBA

TIMU tatu za Tanzania, Simba, Yanga na Azam FC, zimealikwa nchini Ufaransa kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki dhidi ya timu za Ligi Daraja la Kwanza nchini humo ‘League 1’.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage, mechi hizo za kirafiki zitafanyika kati ya Julai na Agosti kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania hapo Agosti 21.

KIKOSI CHA YANGA


Kaijage alisema tayari wameziarifu klabu husika kuhusu mwaliko huo ili ziweze kufanya maandalizi.

Aidha, Kaijage alizitaja miongoni mwa timu za League 1, zilizoonyesha nia ya kucheza na timu za Tanzania ni Auxerre, Soux, Nice, Life na Rens.


KIKOSI CHA AZAM

Comments