RAHMA AL KHAROOSI:MWANAMAMA ALIYEILETEA MABADILIKO TWIGA STARS


“NIMEDHAMIRIA kuwainua wanawake wa Tanzania kwa namna moja ama nyingine ili kutimiza adhama yetu ya kutaka haki sawa na pia kutokuwa wategemezi”.


Hiyo ni kauli ya Rahma Al Kharoosi, rais wa RBP Oil Industrial Technology Tz Limited inayojihusisha na uingizaji wa mafuta na uchimbaji wa madini, ambaye pia ni mlezi wa timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’.

Kwa kipindi cha miaka mitatu tu Rahma ameweza kujijengea jina hapa nchini na hiyo inatokana na mchango wake anaoutoa kwa jamii na hasa wanawake katika sekta mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa mwezi  Mei Rahma alitoa mil.10 kwa Twiga Stars kwa ajili ya maandalizi ya mechi yake dhidi ya Eritrea na matunda yalionekana baada ya timu hiyo kushinda mabao 8-1.

Aidha anatarajiwa kuipelekea timu hiyo nchini Marekani ambapo itapiga kambi maalum ya wiki mbili na kujiandaa na fainali za Afrika kwa wanawake zitakazopigwa Afrika Kusini mwezi Septemba.
Kama hiyo haitosha, Rahma alitoa mil.12 kwa waandaaji wa shindano la Miss Dar Intercollege 2010 kabla ya kutoa mil.5 kwa taasisi ya Tanzania Mitindo House (TMH) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo Gezaulole, Kigamboni Dar es Salaam.
Rahma anasema amelenga zaidi kuisaidia jamii na hasa wanawake kwani bila kunyanyuana wenyewe kwa wenyewe haitatimiza mikakati ya haki sawa kwa wote.
“Nimesukumwa zaidi kusaidia wanawake wenzangu kutokana na kwamba wengi wetu hatupendani, kama mmoja wetu atabahatika kuwa na uwezo wa kifedha inakuwa ngumu kuwapa nafasi ama mwanga wenzake wa nini cha kufanya ili afanikiwe”Anasema.
Akitolea mfano kwenye soka na urembo Rahma anasema “ndio kwanza tumeanza kupiga hatua kali katika sekta hizo sasa muhimu kwa wenye uwezo kusaidia ili kusukuma zaidi gurudumu hilo na kisha baadaye mafanikio yatapatikana”.

Anaongeza kuwa mafanikio ya kitu chochote hayawezi kutimia bila kuwekeza fedha hivyo ametoa wito kwa wadau wa sekta ya urembo, soka na vitu vingine kuwekeza kwa kiwango kinachostahili.

Rahma mama wa watoto wanne pia anamiliki kampuni ya New Forest amabyo inajihusisha na masuala ya Mazingira na upandaji miti iliyopo mjini Iringa na nchini Uganda.
Akiwa ni mzaliwa wa Singida kutoka katika ukoo wa mtemi Senge, Rahma alipata elimu ya msingi katika shule ya Imeri iliyopo Nzega kabla ya kwenda uarabini na kujiunga na elimu ya juu na kisha kusomea kozi ya Accident&Emergence kwa miaka minne na baadaye kufanya kazi katika hospitali ya Khola kati ya mwaka 1987- 1993

Comments

  1. dina huyo mama ananguo nyingine zaidi hizo maana kila story yake katinga nguo hizo hizo au picha hiyo ndiyo imetoa mvuto kidogo katika blog zote anazotolewa habari zake nguo ni hizo kulikoni?

    ReplyDelete
  2. Kwani nguo jamani ni nini? kwa maoni yangu huyu mama hanashida na nguo kwani donations zote atoazo zinatosha ku prove her pointuys she's just a simple lady, guys just leave here alone. i like her

    ReplyDelete

Post a Comment