NYAMBAYA:ANAYETAKA YANGA TISHIO AFRIKA


NYAMBAYA
KUFANYA vibaya kwa Yanga katika michuano ya Afrika ni kero kwa wapenzi wa timu hiyo- na wengine sasa wameamua kuingia madarakani ili kupambana na hali hiyo, kuhakikisha klabu hiyo inakuwa mwiba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kom be la Shirikisho.


Miongoni mwa wanaokerwa na hali hiyo ni Lameck Nyambaya, ambaye ameona kuumia akiwa pembeni si dawa, bali kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama wenzake wa klabu hiyo, kupambana na hali hiyo.

Nyambaya anagombea moja kati ya nafasi nane za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, katika uchaguzi utakaofanyika Julai 18, mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Sabasaba mjini Daer es Salaam, akipambana na watu 27, baada ya Dk Godfrey Luhago kujitoa.

Akizungumza na Sayari mjini Dar es Salaam juzi, Nyambaya anasema dhamira yake akipata nafasi ya kuwa kiongozi Yanga atajali haki za wachezaji wazawa katika timu hiyo.

Nyambaya anasema hatua hiyo itasaidia kukuza na kuendeleza soka la Tanzania linalosaka namna ya kutinga Kimataifa.

Sambamba na hayo pia ana machungu na klabu kubwa kama Yanga ikiwa na maendeleo hafifu yakiwemo mashindano ya Kimataifa Yanga haifanyi vizuri.

“Inasikitisha Yanga ikishiriki mashindano ya Kimataifa kuishia hatua za mwanzo wakati timu wanazocheza nazo ni za kawaida kabisa.

Anasema Yanga ina mfadhili bora, kocha mzuri, wachezaji wazuri ambako tatizo liko katika uongozi ambao hauna mwelekeo katika kuiendeleza timu hiyo.

“Inatakiwa tuwasaidie wachezaji wetu wa Tanzania ambao ndio wataitangaza Tanzania katika medani ya Kimataifa kama zilivyo nchi zilizoendelea,” alisema Nyambaya.

Nyambaya anaomba ridhaa ya wanachama wa Yanga kupitisha jina lake kuwania uongozi wa Yanga.

Anasema Yanga si ya mtu mmoja bali ni ya wanchama ambako atahakikisha uwazi katika mapato na matumizi, Mikutano ya mara kwa mara ili kuwapa wanachama nafasi ya kutoa tathimini za timu.

Kwa kuwa ni kijana atazungumza na wachezaji wa Yanga na kusikiliza matatizo na mafanikio yao, hivyo anaomba apewe kipaumbele.

Anaelezea uzoefu wake katika michezo aliwahi kucheza soka la shule za Msingi (UMISHUMTA) na Sekondari (UMISETA) kabla ya kucheza ligi daraja la kwanza katika timu ya Maji Mara.

Akiwa Dar es Salaam aliteuliwa katika Kamati ya rufaa na nidhamu ya Chama cha soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA) (Mwaka 2002-2005).

Mwaka 2007 aliteuliwa katika Kamati ya ushindi ya mashindano ya vijana chini ya miaka 17 (Copa Coca Cola) wakati mwaka 2008 alijitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania ujumbe katika Shirikisho la soka Tanzania (TFF) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa soka Tanzania (FRAT) Omar Abdulkadir na Muhsin Balhabou.

Anaendelea kueleza kwamba kwa sasa ni Meneja wa timu ya vijana ya Mkoa wa Pwani.

Nyambaya alizaliwa Agosti 25 1978 Wilayani Musoma ambako baba yake mzazi Nyambaya Misonga ni mstaafu wa serikali na mama yake Anne Nyambaya ni mwalimu.

Alisoma elimu ya msingi kuanzia mwaka 1988-1994 katika shule ya msingi Serengeti mwaka 1995-1998 alipata elimu ya sekondari katika sekondari ya Nsumba Mwanza.

Alipata diploma ya ualimu mwaka 1999-2001 kabla ya kuajiriwa na kampuni ya Switch Trade ya Dar es Salaam.

Mwaka 2003 aliteuliwa kuwa Meneja Utawala wa kampuni hiyo, mwaka 2005 Misonga Md Misonga kabla ya mwaka 2008 Nyambaya Logistic.

Comments

  1. Hi dina mimi nakukubali unaouwezo mkubwa na unajua kupangilia mambo ila nakuomba kuhusu picha naomba usizikuze sana kwani zinaumiza macho lakini mwanzo simbaya unatisha uko juu ni mimi mtu wako wa saudia arabia hongera mama.Tupo pamoja.

    ReplyDelete

Post a Comment