NDIMBO AREJESHEWA USEMAJI SIMBA

CLIFFORD NDIMBO

KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba imemrejesha aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo CLIFFORD 'MARIO' NDIMBO.

Mmwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Ndimbo atapata ajira rasmi baada ya kipundi cha uangalizi cha miezi mitatu ambapo atakuwa akifanya kazi chini ya Ofisa Tawala mpya, Evodious Mtawala.

RAGE, MWENYEKITI WA SIMBA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI

Comments

  1. Ndimbo ndio anastahili kuwa Msemaji wa Simba na si mwingine kwa sababu anajua kuishi na wenzake katika masuala ya habari, lakini kama mngemng'ang'ania mliyemtaka Simba ingekuwa si kama ile ya Ndimbo nadhani si mlishamuona

    ReplyDelete
  2. Hata hayo majaribio mliyompatia sioni maana yake kwa sababu Ndimbo alishakuwa Ofisa Habari ambaye aliweza kuendesha gurudumu la Simba, mwacheni afanye kazi na si majaribio kama mnavyomtaka

    ReplyDelete
  3. Mimi nimefurahishwa na Simba kumrejesha Ndimbo kuwa Ofisa Habari wa Simba kwa sababu sikuona maana ya kumnyang'anya nafasi yake wakati kipindi kilichopita hakuwa na kashfa wala kusema sema hovyo zaidi ya kufanya kile alichoambiwa na uongozi wake.

    ReplyDelete

Post a Comment