MSEMAJI SIMBA KUTANGAZWA J3

MTAWALA
KAMATI  ya utendaji ya klabu ya Simba inatarajiwa kukutana kesho jumapili na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kuteua jina la atakayekuwa msemaji wa klbau hiyo ambaye atatangazwa rasmi j3.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema kwamba msemaji huyo atakayeajiriwa na Simba atakuwa akifanya kazi chini ya ofisa tawala wake mpya Evodious Mtawala.

Aidha, Rage alisema wachezaji wa simba wataanza mazoezi ya viungo j3 katika moja ya vituo vya mazoezi 'gym' huku wakisubiri kurejea kwa kocha wao mkuu Patrick Phiri aliyekuwa kwao kwa likizo baada ya kumalizika kwa msimu uliopita wa ligi

Comments