MGOMBEA UJUMBE YANGA AJIENGUA

JAJI MKWAWA, MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI YANGA
MMOJA ya wagomvea wa nafasi ya  Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Dr. David Luhago amejiengua katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa klabu hiyo utakaofanyika Julai 18 katika ukumbi wa PTA uliopo ndani ya viwanja vya Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema  Luhago alifikia hatua hiyo kwa sababu zake binafsi ambazo hakupenda kuzieleza ambako atawasilisha taarifa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji John Mkwawa na katika kinyang’anyiro hicho wamebaki wagombea 28 wa nafasi ya Ujumbe.
Kwa upande mwingine Yanga imekata likizo ya wachezaji wake kutoka  15 hadi julai 10 ili kuweza kujiandaa na ziara ya kimichezo nchini  Ufaransa.

Comments