MARLAW KUKAMUA BILICANAS KESHO

MARLAW

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Marima Lawrance ‘Marlaw’ leo anatarajiwa kutumbuzi katika ukumbi wa Club Bilicanas kupitia usiku wa ‘Bongo Staz Nite’.

Mbali na kutoa burudani Marlaw atatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zake mpya zilizomo kwenye albamu yake ya pili ‘Bidii’ hivyo amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Marlaw anayetamba na kibao chake cha ‘Pipii Pii’, sambamba na vile vya zamani ‘Bembeleza’, ‘Rita’, ‘Busu la Pinki’ na nyinginezo amesema amejipanga kwa shoo ya uhakika ili kuweza konga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza ukumbini hapo.

Usiku wa Bongo Staz urindima kila jumapili na kupambwa na wasanii wanaotamba katika muziki wa bongo fleva ambapo tayari wasanii kama Ali Kiba, Hussin Machozi, Ay, Mwana FA, Chegge, Dully Sykes, Barnaba, Lunah, Mataluma, Tox Star na wengine waliwahi kutumbuiza.

Comments

  1. mwambie huyu jamaa aache ubishoo akalee mtoto wake

    ReplyDelete

Post a Comment