MADA MAUGO AMSTAAFISHA MATUMLA



BONDIA Mahiri hapa nchini Rashid Matumla ‘Snake Man’ juzi usiku alitangaza rasmi kutundika daluga baada ya kupokea kipigo cha pointi 98-95 dhidi ya Mada Maugo.




Matumla ambaye ni bondia aliyewahi kufanya makubwa katika medani ya ngumi hapa nchini alifikia hatua hiyo baada ya miaka kadhaa kushauriwa kuachana na mchezo huo kutokana na umri kumtupa mkono.


MADA MAUGO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI NWA HABARI MARA BAADA YA KUTWAA UBINGWA KWA KUMTWANGA MATUMLA

Awali ilikuwa atangaze kutundika daluga kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya bingwa wa Tanzania, Francis Cheka pambano lililochezwa mwaka juzi kabla ya miezi michache kurudiana.


Katika pambano hilo Matumla alipata tabu kutoka kwa kijana huyo anayewania ubunge katika jimbo la Rorya, vipigo alivyoanza kuviopata kuanzia raundi ya pili.


Pamoja na kuvurumishwa mangumi na kijana huyo pia aliweza kutumia mianya ya kumshambulia kijana huyo mara kadhaa.


Katika mapambano ya utangulizi Abdallah Mohamed alitoshana nguvu na Said Zungu kwa kura 39-39, Said Aziz alikwenda sare ya pointi 39 dhidi ya Faraj Majia.

Comments