KIFUKWE, FALCON WAREJESHWA KINYANG'ANYIRO YANGA

KIFUKWE KUSHOTO AKIWA NA MFADHILI WA YANGA, YUSSUF MANJI

KAMATI ya Uchaguzi  ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewarejesha katika kinyang'anyiro cha kuwania uongozi wanachama wawili wa Yanga waliokuwa wakiwania nafasi ya Uenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na Abeid Falcom.

DEo Lyatto, Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema wameamua kuwarejesha wanachama hao baada ya kuridhika na utetetezi wao kupitia rufaa zao walizowasilisha na wanachama hao kupingwa kuenguliwa na kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa.

Comments