FASHION 4 HEALTH BLACK & GOLD GALA NITE YAFANA



























JOHN MHINA AKIONGOZA TANZANITE BAND

ZAIDI ya sh milioni 10 zimepatikana katika onyesho maalumu la mavazi la ‘Fashion 4 Health Black and Gold Gala nite’ lililofanyika kwenye Hoteli ya Zanzibar Serena Inn visiwani hapa juzi.


Onyesho hilo lilikuwa maalumu kwa ajili kukusanya fedha zitakazosaidia ukarabati wa hospitali ya wagonjwa wa akili iliyopo visiwani hapa.

Katika onyesho hilo lililoandaliwa na Explore Zanzibar, mbali ya maonyesho ya mavazi, kulifanyika mnada wa vitu mbalimbali.

Pia mbunifu wa mavazi, Mustafa Hasanali alizindua mavazi yake mapya yakibatizwa jina la ‘Karafuu’, ambako pia wabunifu wa mjini hapa, Farouque Abdela na Mago Esat Africa nao walionyesha kazi zao.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa Explore Zanzibar kuandaa onyesho la hisani kwa ajili ya kupata fedha za kusaidia hospitali hiyo, ambako hutumika katika kuboresha vitu mbalimbali hospitalini hapo.

Onyesho hilo lililopambwa na bendi ya muziki wa dansi ya Tanzanite, lilidhaminiwa na Vodacom Foundation, PSI Tanzania, Zanzibar Serena Inn, 361 Degree, Vayle Spring na Mustafa Hasanali.

Comments