COSOTA YAUPIGA STOP WIMBO 'KAFARA'

MWIMBAJI WA WIMBO HUO, ABUU FLAVA


CHAMA cha haki miliki Tanzania (COSOTA) kimezuia kupigwa kwa wimbo wa msanii chipukizi wa Bongo Flava Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’, ujulikanao kama ‘Kafara’, imefahamika.



Hatua hiyo inafuatia chipukizi mwingine wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ kupeleka mashitaka cosota akidai kuwa Tanzanite amenakili wimbo wake wa ‘Mbagala’.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juzi Tanzania ambaye pia anajulikana kama Abuu Flava alisema kabla ya kurekodi wimbo huo aliongea na Diamond na kumuomba kufanya hivyo, alimkubalia lakini anashangaa baada ya kutoka akaenda kushitaki Cosota.


Alisema licha ya Diamond kuitwa katika vikao vya usuluhishi cosota alikuwa hatokei na mwishowe maamuzi yakatolewa, hata hivyo anasema amekubaliana na maamuzi hayo na hana kinyongo chochote.


Akienda mbali zaidi, Tanzanite alisema kilichofanya Diamond ageuke ni baada ya kuona ‘Kafara’ ni mzuri kuliko ‘Mbagala’ ndiyo maana ameingiwa na hofu, lakini hata hivyo amejipanga kikamilifu katika medani ya muziki na anatarajia kutoa nyimbo bomba zaidi.

Comments

  1. MIMI BINAFSI SIJUWI KWA NINI AMEPIGIWA MARUFUKU WIMBO WAKE. KAMA MAELEZO NI KWELI YA KUWA AMEPIGWA MARUFUKU KWA KUWA ATI BEATS ZINAFANANA NA ZA WIMBO MBAGALA1 HIYO SI SAHIHI KABISA, HATI MILIKI HAIKO HIVYO MAHALA POPOTE PALE DUNIANI. NINGEELEWA KAMA ALIURUDIA WIMBO KAMA ULIVYO PAMOJA NA MANENO YAKE LAKINI BEATS TU HIYO SI SAHIHI NI MAONEZI NA UTAFSIRI MBAYA WA SHERIA YA HAKI MILIKI. KUNA NYIMBO NYINGI TU HAPA DUNIANI ZINAFANANA BEATS BASI WATU WANGESHITAKIANA SANA TU.

    ReplyDelete
  2. Dina, picha zimetoka vizuri. Nashauri pia uweke 'contacts' za blog hii, k.m. e-mail, simu (si ya binafsi) ambazo zitawaruhusu wasomaji wawasiliane na blog; 'profile' yako (japo sentensi moja) na mwongozo/kanuni za jumla. Idrisa.

    ReplyDelete
  3. Asanteni kwa ushauri wadau, nitufanyia kazi kwani naendelea kuisuka blogu hii, endeleeni kuperuzi,Tupo pamoja

    ReplyDelete

Post a Comment