BONGO FLEVA IMEINGIWA NA MDUDU GANI?

BIFU za hapa na pale katika muziki wa bongo fleva zilitulia kiasi lakini sasa hivi zinaanza kuchipuka taratibu kwa namna moja ama nyingine, Unajua?

Hivi karibuni kumeibuka na taarifa za baadhi ya wasanii kudai kunakiliwa nyimbo zao, midundo nakadhalika, kiasi ambacho kinaleta taswira kwamba kuna msigano baina yao.

Mfano ni Diamond kulalamika kunakiliwa kwa wimbo wake Mbagala, ambapo 'Photocopy' yake inajulikana kama 'Kafara' ulioimbwa na Tanzanite, Diamopnd alikuja juu na kushitaki COSOTA ambayo mwisho wa siku iliupiga marifuku wimbo huo kupigwa katika redio stations.

Huku hiyo ikiendelea, akaibuka msanii mwengine tena chipikizi akatoka na wimbo 'Tatizo Kwetu Tandale'.

Kabla hiyo haijasahalika wiki iliyopita msanii Nazir Ally  'Naz D; kutoka Visiwani Zanzibar naye aeibuka na kudai kuwa Beat ya wimbo 'Usije Mjini' uliombwa na AY & FA ni mali yake kwani aliutengeneza chini ya mtayarishaji Pancho, lakini mtayarishaji huyo hakufanya ustaaarab na kuitoa kwa wakali hao wa bongo fleva.

Pamoja na yote Naz D ameamua kusamehe na kujipanga upya kwania anaamini anauwezo wa kubuni kitu kingine kikali zaidi ya hiko.

 Hiyo ni mifano tu midogo, lakini kesi kama hizo ni nyiungi sana na haileweki kama ni njia ya wasanii kutaka kutoka amatatizo lipo kwa watayarishaji ama la?.

Kwa upnade mwingine si jambo la ajabu kwa vitu kama hivi kutokea kwani kwa wenzetu walioendelea katika medani ya muziki tumekuwa tukishuhudia nyimbo kadhaa zikinakiliwa zaidi ya mara tatu lakini ni mara chache kumekuwa na kelele .

Kikubwa ni kwa wasanii kuelewana wenyewe kwa wenyewe, pia watayarishaji kuheshimu kazi zao na za wasanii kwa kutotumia nafasi walizonazo kuwabeba au kuwakandamiza wengine.

Pia wasanii wazoefu hawana budi kuwasaidia chipukizi kwa hali yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kupunguza matatizo ya namna hiyo.

Ni hayo tu wadau

Comments