BHINDA ATAKA WANAYANGA KUTOFANYA MAKOSA

MOHAMMED BHINDA

MGOMBEA wa nafasi ya uujumbe katika klabu ya Yanga, Mohamed Bhinda amewataka wanachama wa Yanga kuchagua viongozi bora na wenye mapenzi ya dhadi ya klabu hiyo na si kuangalia sura.


Akizungumza jijini jana, Bhinda alisema ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kutoakana na kuona viongozi waliopita wanaongoza ndivyo sivyo hali inayofanya klabu kudidimia hivyo amewaomba wanachama kumpa kura za kumuwezesha kutwaa nafasi hiyo ili kuiletea mafanikio Yanga.

Aliongeza kuwa iwapo atafanikiwa kushika nafasi hiyo atarejesha umoja na mshikamano baina ya viongozi an wanachama, kuisadia klabu kujiendesha yenyewe kupitia miradi mbalimbali itakayoiingizia fedha hivyo kuondoa utegemezi sambamba na kumpunguzia mzigo mfadhili wao, Yussuf Manji.

Katika nafasi hiyo, BHinda anachuana na Isaac Mazwile,Lameck Nyambaya, Theonest Rutashoborwa, Charles Mugondo, Robert Kasela, Ally Mayai, Edger Fongo, Evance Matee, Yussuf Yasin, Shaban Mohamed, Omary Ndula, Atufwigwegwe Mwakatumbula, David Peter, Majid Simba na Mzee Yusuf.

Wengine ni Ramadhan Kampira,Jackson Maagi, Mwinyi Mangara, Hamis Ambari, Paul Malume, Sarah Ramadhan, Salim Rupia, Titto Ossoro, Pascal Kihanga, Ismail Idrissa, John Mayala, na George Manyama

Comments