TAMASHA LA MTEMI MIRAMBO LITAKUWA JULAI 16-18

MENEJA WA BIA YA SAFARI PAMOJA NA BALIMI ,FIMBO BUTALLAH KULIA NA MRATIBU WA TAMASHA LA MTEMI MIRAMBO, AMON MKONGA WAKIONYESHA VIPEPERUSHI KUHUSIANA NA TAMASHA HILO.



KAMPUNI ya Chief Promotions imeandaa Tamasha la Ngoma za utamaduni lijulikanalo kama 'MTEMI MIRAMBO' likiwa na  lengo la kukuza sanaa na kuvitangaza vikundi vya ngoma vilivyopo katika mkoa wa Tabora.


Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni hiyo, Amon Mkonga tamasha hilo litaanza kufanyika katika viwanja vya chipukizi Tabora Tarehe 16 - 18 Julai,2010 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
Siku hiyo shughuli mbali mbali zitafanyika kama vile maonyesho ya ngoma za asili,Sarakasi,Ngonjera na Nyakula vya asili.mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Moshi Mussa Chang'a.

Tamasha hili linakuja kwa udhamini mkubwa toka kwa kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Balimi,Bodi ya Utalii (TTB),Zain Tanzania na Merina Investment.

Chief Promotions imesajiliwa mwaka 2003 na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Baadae Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,na imefanya kazi na Mashirika mengi tu yakiwemo ya Umoja wa Matiaifa (UNAIDS,WHO,UNDP) na pia imefanya kazi na TBL,NSSF,TACAIDS na mengine mengi.


MAWASILIANO:
Amon Mkonga,
Mkurugenzi Mtendaji,
0755 638004/0655 638004
dramontz2002@yahoo.com
http://www.chiefpromotionis.or.tz/

Comments