SITA WAENGULIWA KUWANIA UONGOZI YANGA

MSEMAJI WA YANGA LOUIS SENDEU

BAADHI YA WANAHABARI

KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Yanga imewaangua kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa klabu hiyo wanachama sita waliojitokeza kuchukua fiomu za kuwania nmafasi ya ujumbe katika uchaguzi uliopangwa kufanyika julai 18.


Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kamati ilikutana juzi na kufanyia uhakiki fomu za wagombea na hao sita walioenguliwa hawakuwasilisha vivuli vya vyeti vyao.

Sendeu aliwataja wagombea hao kuwa ni Seif Mohammed, Saburi Saburi, Edson Mandemane, Abas Bomba, Awadhi Mrido na Ahmed Mamba.

Alisema kutokana na mchujo huo wagombea sita watachuana katika nafasi ya uenyekiti, wanne wa nafasi ya makamu mwenyekiti na 30 katika nafasi ya ujumbe na kuanzi leo hadi juni 26 itakuwa ni kipindi cha kuwasilisha pingamizi.

Kwa mantiki hiyo wagombea waliobaki ni pamoja na Francis Kifukwe, Wakili wa kujitegemea Llyod Nchunga, Kanali Mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe, Abeid Falcon, Mbaraka Igangula na Edgar Chubira (mwenyekiti),Davis Mosha, Hashim Lundenga, Ayoub Nyenzi na Constatine Maligo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu katika uongozi wa marehemu Rashid Ngozoma Matunda wanaowania makamu mwenyekiti.

Wagombea wa ujumbe, ni Isaac Mazwila, Theonest Rutashoborwa, David Mlangwa, Majid Simba, Dk. Evance Matee, Fundi mchundo Paul Malume, Paschal Kihanga, Salum Rupia na Ramadhan Kampira,Ismail Idrissa, Omary Ndula, Yusuf Yasin, Ally Mayai Tembele, Ally Bwamkuu, Sarah Ramadhan.
Pia wamo George Manyama, Atufwigwegwe Mwakatumbula, Mwinyi Mangara,Lameck Nyambaya, Robert Kasela, Tito Ossoro,Hamis Ambari, Shaban Mohamed, Mzee Yusuf, Dk.David Luago, Edger Fongo, Mohamed Bhinda, Tony Magale, Jackson Mresi na David Ngarafi.

Kwa mujibu wa ratiba, juni 27 kamati itapitia pingamizi, juni 28 itakuwa ni usaili wa wagombea, juni 29 majina ya wagombea yatatangazwa, julai 5 hadi 7 itakuwa kipindi cha kukata rufaa na kisha kampeni zitafuata.

Katika hatua nyingine Sendeu alisema uongozi umewatema rasmi wachezaji wake Amir Maftah na Jamal Mba, huku wakiendelea na mazungumzo ili kuwabakiza wengine waliomaliza mkataba wa kuichezea Yanga.

mwisho

Comments