REDD'S MISS ILALA WAZURU TBL

MENEJA WA REDD'S, KABULA NSHIMO

WAREMBO WAKIMSIKILIZA MTAALAM WA UBORA WA BIA IKIWA SOKONI, JUSTINO JEKELA


MKURUGENZI WA DAR METROPOLITAN INAYOANDAA MISS ILALA, JACKON KALIKUMTIMA

WAREMBO watakaowania shindano la kumsaka Redd's Miss Ilala 2010 leo wametembelea kampuni ya bia Tanzania (TBL) na kujifunza mbambo mbalimbali ikiwemo vinywaji vinavyzalishwa na kampuni hiyo ambapo moja ya kinywaji zao la TBL ni Redd's Original inayodhamini shindano hilo.








MAMAPIPIRO NA  MKUU WA ITIFAKI WA MISS ILALE, DOUBLE A HATUKUWA NYUMA KATIKA ZIARA HIYO

Aidha warembo hao kesho  watajimwaga kwenye ukumbi wa Club Bilicanas kupitia ‘Usiku wa Mwafrika’ ambako bendi ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ hutoa burudani.


Mkurugenzi wa Dar Metropolitan inayoandaa shindano hilo, Jackson Kalikumtima amesema wakiwa katika klabu hiyo maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kutakuwa na fursa kwa ‘Patron’ wa klabu hiyo kuchagua Miss Popularity Ilala, baada ya warembo kujitambulisha na kutembea kidogo kwenye sehemu ya kuchezea muziki.

Alisema, vigezo vya kumchagua Miss Popularity Ilala vitakuwa ni kupendeza kwa mavazi ya usiku huo, kujitambulisha vizuri na kushangiliwa zaidi na mashabiki na watu watakaokuwa kwenye klabu hiyo.

Warembo watakaoshiriki shindano la Redd’s Miss Ilala wanaendelea vema na tambo za yupi atashinda zimeendelea kuitikisa kambi.


Shindano la Redd’s Miss Ilala 2010 litafanyika Jumamosi Juni 26, ukumbi wa Ubungo Plaza, ambako kiingilio kitakuwa sh 100,000 itakayoambatana na chakula cha jioni na kuangalia mechi ya robo fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia, ‘Business Class’ sh 50,000 na sh 10,000 kwa viti vya kawaida.

Shindano hilo limedhaminiwa na Premium Redd’s Original, Vodacom Tanzania, Aurora Security, Muzasha Tours & Safaris, Fabak fashion, Channel Ten, Magic FM, Sofia Production, Fullshangwe.blogspot, Issa michuzi blogspot, SYSCORP Group, Valye Spring, Clouds FM, Lamada Hotel Apartment na CXC Africa.

Comments

  1. PIGA UWA MWAKA HUU MISS TANZANIA LAZIMA ATOKE ILALA KUNA WAREMBO BOMBA SANA< HONGERA WAANDAAJI KWA KUSAKA WAREMBO WALIOKIDHI VIGEZO,
    MDAU WA UREMBO

    ReplyDelete

Post a Comment