RBP OIL INSUSTRIAL TZ LTD YATANGAZA ZIARA YA TWIGA USA

RAIS WA RBP OIL INDUSTRIAL TECHNOLOGY TZ LIMITED NA MLEZI WA TWIGA STARS RAHMA AL HAROOS AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JANA KUHUSIANA NA ZIARA YA TWIGA STARS NCHINI MAREKANI ITAKAYOKUWA 7 HADI 11 MWEZI AUGUSTI 

WADHAMINI wa timu ya soka ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology Tz Limited wamesema timu kambi maalum ya timu hiyo nchini Marekani itakuwa Augusti 7 hadi 12 mwaka huu.


Ziara hiyo nni mahsusi kwa Twiga kujiandaa kwa fainali zao za kwanza kushiriki za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawawake zitakazofanyika mwezi Septemba huko Afrika Kusini ambapo wameshirikiana na taasisi ya Freedom Washngton ya nchini Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Movenpick,Rais wa kampuni hiyo na mlezi wa Twiga Stars Rahma Al Kharoos alisema maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na ikiwa huko itacheza mechi nne za kirafiki.
Alisema ikiwa nchini Marekani, mchezo wake wa kwanza kati ya hiyio minne utakuwa kwa ajili ya kuisaidia Twiga Stars ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

Kwa upande mwingine Rahma aliiipongeza Twiga Stars kwa kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali hizo walizokuwa wakiwania nafasi kwa muda mrefu, hilo limetimia baada ya kuifunga Eritrea kwa jumla ya mabao 11-4.

Comments