PINGAMIZI 14 ZAWASILISHWA YANGA


ZOEZI la kuwasilisha pingamizi za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga limefungwa rasmi jioni ya leo na pingamizi 14 zimewasilishwa.

Waliowekewa pingamizi ni papmoja Francis Kifukwe, Lyod Nchunga, Mbaraka Igangula, Ali Mwanakatwe wanaowania nafasi ya Mwenyekiti kila mmoja amewekewa pinamizi mbili.

Pia wagombea wa nafasi ya makamu mwenyeki Hashim Lundenga na Costantine Marigo, pamoja na Teofrid Rutashoborwa anayewania nafasi ya ujumbe kila mmoja amewekewa pingamizi moja.

Uchaguzi wa Yanga utafanyika Julai 18

Comments