VIONGOZI TASWA KUCHAGUANA AGOSTI 7,2010

KATIBU MSAIDIZI WA TASWA, AMIR MHANDO
                                                                       
MKUTANO mkuu wa uchaguzi wa chama cha waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA) unatarajiwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi wa Taswa Amir Mhando amewahimiza wanachama kulipa ada ya mwaka kila mmoja ambayo ni sh.20,000 ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni Julai 20.

Alisema kwamba viongozi waliopo madarakani wanahaki ya kutetea nafasi zao isipokuwa Mwenyekiti, Katibu Msaidizi na wajumbe wawili ambao wameongoza kwa vipindi viwili hivyo katiba haiwaruhusu.

GRACE HOKA, MJUMBE WA TASWA
                                               
Mhando alisema zoezi la utoaji na urejeshaji fomu kwa watakaotaka kuwania nafasi mbalimbali litaanza Julai 26 hadi Agosti 2, huku uongozi wa sasa ukipanga kuunda kamati maalum itakayosimamia uchaguzi huo badala ya baraza la Habari nTanzania (MCT).

“Kamati hiyo iatawahusisha waandishi waliobobea kwenye taaluma ya uandishi wa habari na hasa za michezo ambao naamini watakuwa wanawafahamu ipasavyo wagombea hivyo kutopata mkanganyika katika mchakato mzima”,
 
                        'SA VIPI TUTIE NIA TENA AU?                                                   

Comments

  1. hivi hiko chama kazi yake nini jamani, mbona hatuoni wanachokifanya zaidi ya Amir ndio tunamsikia, waandhishi mnakazi ya ikuwatangaza na kutetea wengine si wenyewe hebu mchague sura mpya

    ReplyDelete

Post a Comment