KADUGUDA ATEMBEZA UZI WA SIMBA KUTOKA USA


                                                           UZI NDO HUU

KATIBU Mkuu wa Simba Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’, leo ametemblea kampuni ya Free Media Limited, wachapishaji wa magazeti ya TANZANIA DAIMA  na lile la Michezo SAYARI na ujio wake ulikuwa na lengo la kuzionyesha jezi mpya za klabu hiyo kabla ya kuzikabidhi rasmi kwa uongozi hapo kesho.

Kaduguda amesema jezi hizo zimekuja baada ya kuingia mkataba wa biashara na kampuni ya Nsejjere Sports and Casual Wear, yenye makao makuu yake Washington, Marekani, Novemba mosi 2009 ili kampuni hiyo iweze kuitangaza Simba kitaifa na kimataifa pia kuuza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo.
MAMAPIPIRO PIA SIKUPITWA KUJITUPIA KIDOGO UZI MPYA WA MSIMBAZI NASUBIRIA UJE MZIGO WA WOTE
                                                      
Katika mkataba huo, mbali ya kuipa jezi, lakini pia Simba itanufaika kwa mauzo hayo yatakayofanywa na kampuni hiyo kwa bidhaa mbali mbali.

Alisema kwa mujibu wa taarifa aliyotumiwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Isaac Mayanja tayari bidhaa za Simba zimeshatumwa ziko njiani na zinatarajiwa kufika bandarini baada ya wiki nne na kampuni hiyo italipia kila gharama zote bandarini.
                                                            
HAPA NIKIWA NA MDAU TULLO CHAMBO A.K.A MJESHI, A.K.A SOFAPAKA, A.K.A JABULANI



KADUGUDA KUSHOTO AKIWA NA TULLO
                                                            

                                                     

Comments

  1. mamapipiro unatisha kumbe wewe ni shabiki wa wekundu wa msimbazi?

    ReplyDelete

Post a Comment