JAN B.POULSEN KOCHA MPYA STARS




 KATIBU MKUU WA TFF FREDERICK MWAKALEBELA AKIWATANGAZIA WANAHABARI MRITHI WA MAXIMO

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Mdenmark Jan B. Poulsen (64) kuwa ndiye atakayerithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo katika kuinoa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

Akizumgumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela, alisema kamati ya utendaji chini ya mwenyekiti wake Leodger Tenga ilikutana juzi na kumteua Poulsen kupitia mapendekezo toka kamati ya ufundi.
Alisema, kocha huyo mwenye kiwango cha juu ni mchezaji mstaafu wa kimataifa wa Denmark ambaye amewahi kuzifundisha timu mbalimbali za taifa na kupata mafanikio, pia ana leseni ya kiwango cha juu cha ualimu (Pro License).
Akiwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Denmark alitwaa ubingwa wa Mataifa ya Ulaya katika fainali za mwaka 1992 zilizofanyika Sweden kufuatia ushindi dhidi ya Ujerumani.
Pia amewahi kuwa kocha wa timu za taifa za vijana chini ya miaka 19, 20 na 21 za Denmark, kocha mkuu wa timu za taifa na mkurugenzi wa ufundi wa nchi za Jordan, Singapore na Almenia

Poulsen si tu mwalimu bali pia ni mkufunzi wa walimu wa soka wa kiwango cha kimataifa anayetambuliwa na FIFA na amekuwa akiendesha mafunzo ya walimu wa soka yanayoandaliwa na mataifa mbalimbali duniani

Comments