BARNABA, LINAH ndani ya BILICANAS KESHO



CHIPUIKIZI wanaofanya vema kwenye bongo fleva kwa sasa Barnaba na Linah toka kituo cha Tanzania House of Talent (THT) leo wanatarajiwa kutumbiza katika klabu nmaarufu ya Bilicanas kupitia usiku wa ‘Bongo Staz Nite’.

Akizungumza jana, Barnaba alisema kupitia onyesho hilo atatambulisha wimbo mpya ‘Mwenyekiti wa Kamati’ uliopo kwenye albamu yao ya pamoja na msanii mwenzake Amin ijulikanayo kama ‘njia panda’.

Alisema mbali na utambulisho huo pia ataimba vibao mbalimbali vilivyopo kwenye albamu hiyo ikiwemo ‘Njia Panda’, Wrong Number’, ‘Mbalamwezi’, ‘Mama Vanessa’, ‘Robo Saa’, ‘Soo soo’, ‘Simu ya Kamera’, ‘Nivumilie’, na nyinginezo.

Aidha, Linah naye anayetamba na kibao chake cha ‘Atatamani’ atatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbvo zake mpya ambazo zinatarajia kuwemo katika albamu yake itakayotoka baadaye mwaka huu.

‘Bongo Starz Nite’ inayorindima kila jumapili ukumbini hapo hupambwa na nyota mbalimbali wanaofanya vema kwenye bongo fleva ambapo tayari wasanii wakali wakiwemo Ali Kiba, Chegge, Diamond, Hussein Machozi, Belle 9, Dully Sykes, Mwana Fa, AY wameshatumbuiza.

Comments