AKUDO NDANI YA DOM JULAI 9

BENDI ya Muziki ya dansi ya itafanya nchini Akudo Impact Wanapekecha Pekesha Ijumaa ya Julai 9 itafanya utambulisho rasmi wa Albamu mpya na utambulisho wa wanenguaji wake wapya utakafanyika kwenye Ukumbi wa Polisi Jamii Uliopo Dodoma .

Mratibu wa onesho hilo hilo Zahor Said, alisema kuwa onesho hilo maalum la utambulisho wa albamu inayotwa History No Change, pamoja na wanenguaji wapya ambao wametoka nchini Congo .

Said alisema kuwa onesho hilo maalum litaaanza saa 2 usiku nia ni kuwapa burudani wapenzi wa mkoa wa dodoma na vitongoji vyake.

“Tumejipanga kutoa burudani siku hiyo maalum ya utambulisho Akudo itafanya vitu vya uhakika itatoa vionjo vya wanenguaji wapya ambao Akudo imewachukuwa kutoka Congo ,”alisema Said.

Said alisema katika utambulisho huo kutakuwa na burudani nyingine mbili ambazo zitasindikiza usiku huo ambapo mazungumzo na bendi hizo yanaendelea.
Baadhi ya nyimbo za albamu hiyo ni Ndoa, Umefulia na Ubinafsi na inayobeba albamu hiyo History No Change.

Alisema tamasha hilo limedhaminiwa na CXC Africa , Clouds FM, jane john5blogsport, Shabiby Line na Full Shangwe.

Comments