Yanga yapata mdhamini mdhamini mpya, italamba bil.1.3 kwa mwaka


MDHAMINI WA SASA WA YANGA YUSUF MANJI ALIYEWEZESHA KUPATIKANA KWA MDHAMINI MWENZA

Mdhamini wa klabu ya Yanga, Yusuf Mehbob Manji ameitafutia mdhamini mweza timu hiyo ambapo udhamini wa miaka mitani wenye thamani ya dola milioni tano sawa na bil.6.5 za kitanzania.
Kwa mujibu wa barua ya Manji kwenda kwa mwenyekiti wa yanga Iman Madega, mdhamini huyo ataipatia dola milioni moja kila mwaka.
Yanga pamoja na mahasimu wao wa jadi Simba wanadhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bila ya Kilimanjaro, huku pia kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ikidhamini Ligi kuu bara ambayo Yanga pia inashiriki.

Comments