RBP YAIPONGEZA TWIGA STARS KWA KUIFUNGA ERITREA 8-1

RAIS WA RBP RAHMA AL KHAROOS

MDHAMINI mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania Limited imeipongeza timu hiyo kwa ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Eritrea juzi.
KAIMU KOCHA MKUU WA TWIGA STARS, ROGATIAN KAIJAGE
Ushindi huo mnono kwa Twiga umeiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za Afrika kwa wanawake zitakazopigwa mwezi Septemba huko Afrika Kusini kabla ya timu hizo kuruddiana wiki mbili zijazo ambapo Eritrea wanahitaji kushinda mabao 7-0 ili kuitoa Twiga.
MWAHAMIS OMARY ALIFUNGA MANNE

Akizungumza na waandishi wa habari jana, meneja uendeshaji wa kampuni hiyo Ibrahim Khatrush alisema ushindi huo umetokana na juhudi za dhati za walimu na wachezaji wote wa timu hiyo ambao waliahidi kufanya vema.
ASHA RASHID 'MWALALA' ALIFUNGA MATATU

“Napenda kutoa pongezi kwa niaba ya rais wa RBP Rahma Al Kharoos ambaye kwa sasa yupo nchini NMarekani akiendelea na maandalizi ya kambi ya Twiga Stars pamoja na kutafuta mechi za majaribio zikazochezwa pindi itakapokuwa huko”, Alisema Khatrush.
Ikumbukwe kuwa kampuni hiyo iliipatia Twiga Mil.10 kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya juzi sambamba na kuahidi kuipeleka nchini Marekani timu hiyo kwa kambi ya wiki nne mwezi juni.
NAHODHA WA TWIGA STARS SOFIA MWASIKILI ALIFUNGA MOJA


Naye katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela aliwapongeza wachezaji wa timu hiyo na kushema ushindhi huo ni hamasa kwa timu za wenzao katika michezo yao hivi karibuni kuanzia ile ya wakubwa hadi za vijana chini ya miaka 17 na 20.
Mwakalebela alisema wanatarajia kuipeleka kambini timu hiyo katika sehemu zenye hali ya hewa inayofanana na Eritrea ili kuweza kuzoea hali ya hewa.

Comments