RBP MISS DAR INTERCOLEGGE KUZOA MIL1.5, CLUB BILICANAS YAMWAGA OFA YA MWAKA MMOJ

WAKATI mrembo atakayetwaa taji la RBP Miss Dar Intercollege 2010 akizawadiwa mil.1.5, klabu yenye hadhi ya kimataifa Bilicanas nayo imetoa ofa ya kuingia bure mwaka mshindi wa kwanza hadi wa tatu.
Shindano hilo litakanyika alhamis kwenye ukumbi wa Club Bilicanas ambapo pia mshindi wa nne na watano watapata ofa ya kuingia bure katika klabu hiyo kwa miezi sita huku waliobaki watapewa ofa ya miezi mitatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mratibu wa shindano hilo Silas Michael alisema wameamua kutoa zawadi ya fedha ili ziwasaidie warembo hao katika mahitaji yao ya kielimu.

Alisema mshindi wa pili atapata mil.moja, mshindi wa tatu atapewa 500,000, wa nne 400,000, wa tano 300,000 wakati washiriki waliosalia kila mmoja atapata 200,000.

Aliongeza kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamlika ambapo warembo bado wanajifua kila siku ukumbini hapo chini ya wakufunzi wao Beatrice Lukindo na Bob Rich.

Shindano hilo limedhaminiwa na RBP Oil& Industrial Technology (T) Limited, Tanzania Daima, Club Bilicanas, Redd’s Original, Vodacom Tanzania, Shear Illusion, Dotnata Decorations, Condy Bureau Change, Clouds Fm, Ndege Insurance na Michuzi/Full Shangwe, Jane John 5, Mtaa kwa Mtaa blogspot.

Comments