RBP YAIPA TANZANIA MITINDO HOUSE MILIONI TANO

RAIS WA RBP OIL INDUSTRIAL TZ LIMITED RAHMA AL KHAROOS

KAMPUNI ya RBP Oil Industrial Technlogy Tz Limited imeipatia milioni tano taasisi Tanzania Mitindo House (TMH) kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha michezo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika kwenye hoteli ya Movenpick, Rais wa kampuni hiyo Rahma Al Kharoos alisema msaada huo ni sehemu ya mpango wake wa kuisaidia jamii.

Alisema watoto hao hawana budi kusaidia ili waweze kupata faraja na kujisikia kama watoto wengine ambao wana wazazi wao hivyo kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidiwa.


Kituo hicho kinachojengwa eneo la Gezaulole, Kigamboni kitazinduliwa juni 12 ambapo watoto toka vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima watakuwa wakikitumia katika siku za mwisho wa wiki ama siku za sikukuu.

Naye Mwenyekiti wa TMH inayoundwa na wabunifu mbalimbali wa mitindo hapa nchini, Khadija Mwanamboka alishukuru kwa msaada huo na kusema utatumika kwa lengo lililokusudiwa .

Mwanamboka alisema licha ya taasisi yao kumiliki kitua kinacholelea watoto yatima lakini waliona ni bora kujenga kituo kitakachowakuitanisha watoto toka vituo tofauti kwani hakuna kituo mahususi kwa ajili yao.

Comments