RAHMA AL KHAROOS amwaga Mil 12 Miss Dar Intercollege 2010








RAIS WA RBP OIL INDUSTRIAL TECHNOLOGY TZ LIMITED, RAHMA AL KHAROOS 'OPRAH' AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUTANGAZA UDHAMINI WAKE, KULIA NI MRATIBU WA SHINDANO HILO SILAS MICHAEL



OPRAH AKIWA KATIKA PICHA YA POZI NA BAADHI YA WASHIRIKI


OPRAH

MAMAPIPIRO, ANGELA MSANGI AMBAYE NI MWANDAAJI NA OPRAH TUKIJADILIANA JAMBO

KAMPUNI inayiojihusisha na uingizaji wa mafuta pamoja na madini ya RBP Oil Industrial Technology Tz Limited imetoa mil.12 kwa ajili ya kudhamini shindano la urembo la Miss Dar Inter College linalotarajiwa kufanyika Mei 27 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Movenpick, Rais wa kampuni hiyo Rahma Al Kharoos ‘Oprah’ alisema ameamua kudhamini shindano hilo ili kuendeleza jitihada zake za kuisaidia jamii na hasa wanawake.

Alisema kutokana na umuhimu wa shindano hilo ameona hana budi kuwasaidia kwa hali na mali waandaaji ili kuhakikisha wanafanikisha shindano hilo kikamilifu na hatimaye kuwapata wawakilishi bora watakaowakilisha katika hatua za juu.

Aidha, Rais huyo aliwataka warembo hao kuwa mabalozi wazuri katika jamii kwa kufanya mambo mema sambamba na kusaidia wale wasiojiweza kwani urembo si sura wala mavazi bali ni tabia njema na moyo wa kujitolea.

Naye mratibu wa shindano hilo Silas Michael alimshukuru mdhamini huyo mkuu wa shindano hilo na kusema kuwa fedha hizxo zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiomba wadhamini wengine wajitokeze kudhamini shindano hilo.
Silas alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vema ambapo warembo 15 watakaowania taji hilo wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Club Bilicanas wakinolewa na Beatrice Lukindo.

Aliwataja wadhamini wengine wa shindano hilo kuwa ni pamoja na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd’s Original na Free Media Limited ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari.

Comments