MANJI KUWANUNULIA WANACHAMA YANGA TIKETI ZA KUIONA MECHI KATI YA BRAZIL VS TAIFA STARS

YUSUF MANJI
WANACHAMA wote wa klabu ya Yanga watakaohudhuria mkutano wa marekebisho ya katiba utakaofanyika juni 6 watapewa tiketi za kushuhudia mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya Stars na Brazil.
Ofa hiyo imetolewa na mdhamini mkuu wa klabu hiyo Yusuf Manji ili kuwaopa fursa wanachama hao kwenda kuishangilia Taifa Stars hivyo kuwapa nguvu wachezaji.

Taarifa zilizopatikana  kutoka kwa mdhamini huyo, hatua hiyo inafuatia uongozi kumuomba asaidie kufanikisha mkutano huo ambapo Manji amekubali kugharamia kila kitu.

Aidha, Manji ameamua kununua tiketi za viwango vya 30,000 akiamini pia zitalisaidia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia fedha kwa ajili ya kusaidia gharama za ujio wa Brazil.

Kwa mujibu wa barua ya Manji aliyoiandika jana kwenda kwa katibu mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako, mbali na gharanma hizo pia atagharamia usafiri wa wanachama kutoka klabuni kwenda Bwalo la maofisa wa polisi Oyesterbay utakapofanyika mkutano huo.

Kama hiyo haitoshi, Manji pia ameahidi kugharamia chakula kwa wanachama wopte watakaohudhuria mkutano huo utakaanza kurindima majira ya saa tatu asubuhi.

Comments