KUMEKUCHA MISS LINDI


MISS LINDI 2009 GLORIA BLANCA MAYOWA

Warembo 12 watakaowania taji la Miss Lindi 2010 wataingia kambini kesho kwenye hoteli ya Lindi Oceanic View ambapo watakuwa wakinolewa na Caroline Zayumba tayari kwa shindano linalotarajiwa kufanyika Mei 29 ukumbini hapo.

Mratibu wa shindano hilo, Shah Ramadhan amesema maandalizi mengine yanaendelea ikiwemo mazungumzo na baadhi ya makampuni ili kuweza kudhamini shindano hilo.

Aliwataja wadhamini waliopo mpaka sasa ni pamoja na Lindi Oceanic View, Vodacom Tanzania, kinywaji cha Redd's, Ndanda Spring Water, Mikindani Salt, Kipalata Tailorinmg Mart, BiG Solution, AG Autos na Muhsin General Enterprises.

Comments